Thursday , 26th Jun , 2014

Tofauti ya kisiasa iliyosababisha nchi ya Cyprus kugawanyika sehemu mbili za kaskazini na kusini imetajwa kuwa sio sababu ya kuwazuia vijana wa Kitanzania wanaotaka kwenda kusoma masomo yao ya elimu ya juu nchini humo.

Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Bi. Jennister Mhagama.

Afisa kutoka chuo kikuu cha kimataifa cha Cyprus Profesa Hassan Ali Bicak, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam kufuatia taarifa kuwa chuo hicho hakitambuliki na mamlaka yoyote ya kimataifa ikiwemo pia ndani na nje ya Cyprus na kwamba takribani wanafunzi 200 wa Kitanzania wanaosoma katika chuo hicho shahada zao hazitotambulika.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Profesa Bicak amesema licha ya tofauti za kisiasa zilizosababisha upande wa kaskazini wa nchi hiyo kujiunga na Uturuki bado chuo hicho na vingine vya aina hiyo vinatoa elimu inayotambulika kimataifa ikiwemo tume ya vyuo vikuu nchini TCU.

Aidha, Profesa Bicak amesema mpaka sasa idadi kubwa ya vijana wa Kitanzania wamesoma katika chuo hicho na kupata shahada zinazotambulika kimataifa na kwamba hatua ya nchi hiyo kugawanyika vipande viwili ni ya kisiasa zaidi ambayo haiwezi kuathiri mtiririko wa masuala ya kitaaluma.
…............................