Tuesday , 19th Dec , 2017

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera inahitaji wastani wa uniti elfu ishirini na tano za damu safi ili iweze kukidhi mahitaji wa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ambapo miongoni mwao ni watoto umri chini ya miaka mitano, wajawazito na wapatao ajali.

Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoani wa Kagera Dkt. John Mwombeki baada ya kupokea msaada vifaa mbalimbali ambavyo hutumiwa na watu wanaojitokeza kujitolea damu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Mstaafu Mstapha Kijuu amewahimiza wananchi katika mkoa wa kagera wajenge utamaduni wa kujitolea damu ili waweze kuokoa maisha ya wagonjwa ambao wakati mwingine hupoteza maisha kutokana na sababu ya tatizo la upungufu wa damu katika hospitali hiyo

Msaada wa vifaa vinavyotumika wakati wa kutoa damu umetolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kukiimarisha kitengo cha damu safi na salama cha hospitali hiyo ili kiweze kukusanya damu nyingi itayokidhi mahitaji ya wagonjwa