
Mgeni rasmi katika sherehe hizo za maadhimisho anatarajiwa kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
Uongozi wa mkoa wa Dodoama ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa umeunda kamati ya maandalizi kwa ajili ya sherehe hizo, na maandalizi muhimu tayari yamekamilika.
Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Bilinith Mahenge, ametaja kuwa maonesho hayo yatapambwa na gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama nchini, onesho la vikosi vya Komandoo, kwata ya kimyakimya na gwaride la mkoloni kutoka Jeshi la Polisi .
Kufanyika kwa gwaride la mkoloni katika maadhimisho hayo ya uhuru, itakuwa ni mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake.
Kauli mbiu mwaka huu ni 'Uhuru wetu ni tunu, tuudumishe, tulinde rasilimali zetu, tuwe wazalendo, tukemee rushwa na uzembe'.