Msemaji wa mamlaka ya chakula na dawa TFDA, Gaudensia Simwanza.
Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Uhusiano wa TFDA Gaudensia Simwanza amesema mamlaka itaanza kutoa elimu hiyo kuanzia mwaka wa fedha ujao ambapo kwa sasa wamefanya ukaguzi pamoja na kuteketeza baadhi ya vipodozi hivyo vyenye sumu katika maeneo mbalimbali nchini.
Simwanza, amesema ukaguzi wa vipodozi hivyo umefanyika katika vituo vya mpakani na maduka ya jumla, ingawaje watu wa forodha wamekuwa ni chachu kubwa ya uingizwaji wa vipodozi vilivyopigwa marufuku nchini.