Maeneo ambapo bomu hilo lililipuka
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa upelelezi na makosa ya jinai Zanzibar SACP Yussuf Ilembo ameseme bomu hilo lilitupwa na mtu au watu wasiojulikana ambao walikuwa ndani ya gari lililo kuwa halina namba za usajili katika kikundi cha wananchi waliokuwa pamoja na viongozi wa dini ambao walikuwa wametoka msikitini na wamesimama nje ya gari.
Baada ya kutupiwa bomu hilo kijana mmoja Mohamed khatibu Mkombalaguha ambaye ni mkazi wa Pongwe Tanga aliyekuwa Zanzibar kwa ajili ya Hitima, alifariki hapo hapo na wengine saba akiwemo Sheik Kassim Mafuta kujeruhiwa.
Jeshi la polisi hadi sasa halijakamata mtu yeyote.
Nao baadhi ya majeruhi Ahmed Haidar na mwanawe khalid Ahmed wakiongea na EATV wakiwa wamelazwa hosptali ya Alrahma wamesema hawajui wala hawakumuona mtu ailyerusha bomu hilo wao wameshtukia mlipuko mkubwa majira ya saa mbili na nusu usiku wa jana (Juni 13, 2014).
Hakuna taarifa yeyote iliyotolewa na seriklai wakati hili likiwa ni tukio la pili la kulipuka mabomu mjini Zanzibar katika kipindi cha miezi minne.
Matukio mengine yalitokea katika mwezi Februari ambapo mabomu zaidi ya matatu kuyalilipuka katika mgahawa wa Mercury na mabomu mawili nje ya lango kuu la kanisa la Angilkana Mkunazini na hadi sasa hamna mtu aliyekamatwa.