Wednesday , 11th Jun , 2014

Msanii mkali wa vichekesho kutoka Uganda, Anne Kansiime amepata shavu jingine kubwa huko nchini Kenya kwa kuchaguliwa kuwa balozi wa kampeni zenye lengo la kuhamasisha wakenya kujifunza zaidi kuhusiana na sera za bima.

Anne Kansiime akifanya yake stejini

Kampeni hizi zimepatiwa jina la Question ambapo Kansiime kwa kutumia uwezo na kipaji chake anatarajiwa kusaidia kuwapatia wananchi msukumo wa kuuliza maswali bila aibu ili kuongeza uelewa juu ya huduma za bima.

Msanii huyu katika shughuli hii anaungana na mastaa wengine wa filamu kutoka Kenya, akiwepo Dennis Mugo maarufu zaidi kama OJ na Francis Njenga aka Mogaka.