Wednesday , 11th Jun , 2014

Mamlaka ya elimu nchini Tanzania imesema bado kuna mahitaji ya vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini, ikiwemo vitabu, pamoja na mabweni ambayo yatasaidia wanafunzi hao kuishi kutokana na umbali mrefu wanaotembea kwenda shule.

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dkt Shukuru Kawambwa.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Meneja Uhamasishaji na rasilimali kutoka Mamlaka ya Elimu nchini TEA Bw. Charles Mapima wakati alipokuwa akizungumza na East Africa Radio kuhusu changamoto zinazowakabili wanafunzi na mpango mkakati wa TEA katika kuzisaidia vifaa shule za sekondari za jijini Dar es salaam na nje ya jiji la Dar es salaam.

Amesema hali halisi ya mahitaji katika sekta ya elimu kwa shule za msingi ni pamoja na kuwepo kwa uhaba wa vyoo, vyumba vya madarasa, maabara na maktaba na amezitaka taasisi, pamoja na mashirika yanayoguswa na changamoto hizo kusaidia kwa lengo la kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.