Friday , 6th Jun , 2014

Mwanadada Cindy Sanyu, Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, ameweka wazi kuwa, sababu ya kuachana na Mario ambaye ni baba wa mtoto wake, ni kutokana na kuona hana malengo ya kuhalalisha mahusiano yao kwa kumuoa.

Cindy na mpenzi wake Mario wakiwa na mtoto wao

Cindy ambaye amekuwa katika mahusiano na Mario kwa miaka 10, katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni amefunguka kuwa, baada ya kutengana na Mario, ameweza kukutana na Ken ambaye naye alikuwa ametengana na mama mtoto wake, na hivyo baada ya kuelewana wakaanzisha safari mpya ya mapenzi.

Cindy ameendelea kusisitiza kuwa, hakusababisha Ken kutengana na mama mtoto wake, na kwa sasa staa huyu yupo katika kesi ya haki ya malezi ya mtoto aliyezaa na Mario ambayo itasikilizwa tena mahakamani Juni 26.