Saturday , 1st Mar , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Jux kutoka Wakacha, kufuatia tetesi zisizo rasmi ambazo zimekuwa zinaendelea kwa muda kuhusiana na mahusiano yake ya kimapenzi, huku akitajwa kuwa na mahusiano na mwanadada Jackie Cliff, ameamua kutoa maelezo yake rasmi juu ya ishu nzima ya mahusiano yake ilivyo.

Jux amesema kuwa, tofauti na wengi ambavyo wamekuwa wakifikiri, Yeye pamoja na Jackie Cliff wamekuwa ni marafiki wa karibu tu, huku akisema kuwa kwa sasa ana mpenzi mwingine ambaye hakupenda kumuweka wazi, na pia amesema hawezi kuongelea kuwa mwanadada huyo yupo wapi kwa sasa.

Jux pia akafafanua kuhusu kazi yake mpya Nitasubiri ambayo itatoka hivi karibuni, na kama ina uhusiano wowote na story za Jackie kukamatwa huko China ambapo amesema ni watu wameunganisha matukio ingawa ni kweli kuwa wimbo huu unatokana uhalisia wa wakati ambao amepitia/anapitia.