Tuesday , 27th May , 2014

Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba imemuondoa aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais wa klabu hiyo Michael Richard Wambura kutokana na kutokuwa mwanachama halali wa Simba

Michael Wambura wakati akirudisha fomu ya kugombea

Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba imemuondoa aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais wa klabu hiyo Michael Richard Wambura baada ya kuwekewa mapingamizi kadhaa na mojawapo kuonekana ni sahihi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Dr Damas Daniel Ndumbalo amesema Wambura ndiye mgombea pekee aliyetemwa katika mbio hizo na sababu kubwa ni suala la uanachama wake kuwa na mashaka, kwa kuwa amewahi kuvuliwa uanachama lakini hakuna kikao chochote kilichowahi kumrudishia uanachama wake.

Kamati ya uchaguzi ya klabu ya soka ya Simba imesema wagombea 31 kati ya 41 wamewekewa wa nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu Simba ambapo kamati imekutana mwishoni mwa juma lililopita na Mgombea mmoja kuenguliwa huku wengine 30 masuala yao yakitakiwa kufikishwa katika kamati zingine.

Akizungumzia maamuzi hayo, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba Dr. Damas Ndumbaro amesema hakuna mtu aliyeondewa kwakuwa maamuzi yao yamezingatia katiba na kanuni za uchaguzi wa klabu hiyo.

Maamuzi hayo yamepelekea Mgombea wa nafasi ya Urais wa klabu ya soka ya Simba Michael Wambura kuenguliwa katika kinyang'anyiro hicho baada ya kamati ya uchaguzi ya klabu ya simba kutangaza kuenguliwa kwake kutokana na katiba na kanuni za uchaguzi

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa kabu ya Simba Dr Damas Ndumbaro amesema mgombea mmoja pekee yaani Michael Wambura yeye ameondolewa kwa sababu kubwa ya kutokuwa mwanachama halali wa klabu hiyo baada ya kusimamishwa uanachama kutokana na kupeleka masuala ya michezo mahakamani na mpaka sasa kamati ya uchaguzi haina taarifa yoyote ya kubatilishwa maamuzi hayo.

Uchaguzi wa Klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Juni 29 ambapo wagombea wa nafasi ya Uraisi akibakia Evance Aveva na Andrew Tupa