Monday , 26th May , 2014

Ukarabati mkubwa wafanywa katika viwanja vya gofu katika klabu ya Lugalo na sasa viwanja hivyo viko tayari kutumika kwa hali ya hewa ya aina yoyote

Mmoja wa wachezaji wa gofu katika michuano ya wazi ya Lugalo

Uongozi wa klabu ya gofu ya Lugalo jijini Dar es salaam umesema miundombinu ya kuchezea katika viwanja hivyo iko vizuri tayari kwa mashindano mbalimbali ya gofu

Afisa tawala wa viwanja hivyo Lambart Ngonyani amesema awali April 12 na 13 kulikua kufanyike michuano ya wazi ya Lugalo lakini iliahirishwa kutokana na miundombinu kuwa mibovu lakini hivi sasa viwanja hivyo vimekua katika ubora wa hali ya juu tayari kwa mashindano yajayo ya wazi ya Lugalo ambayo yataanza mwezi ujao wachezaji mbalimbali toka klabu zote hapa nchini

Lambart amesema mashindano hayo ambayo yatakua na zawadi za aina tofauti yatafanyika kwa siku mbili kuanzia june 8 na 9 na hivyo amewataka wachezaji wote ambao wanataraji kushiriki michuano hiyo kufanya maandalizi ya kutosha kwakua wao kama Lugalo klabu timu yao imejiandaa vema kuhakikisha inatoa ushindani katika michuano hiyo ambayo itafanyika katika viwanja vyao vya nyumbani.