Bonge la Nyau ambaye kwa sasa anatamba na video yake mpya ya Uaminifu ambayo amemshirikisha Msanii Ally Kiba, amesema kuwa mbali na muziki, yeye pia hujihusisha na biashara mbalimbali ikiwepo ya nguo ambazo huzitoa nnje ya nchi.
Msanii huyu pia akagusia ishu ya Gharama za video yake ya “Uaminifu” ambayo amesema kuwa imemngarimu shilingi milioni 2 tu kuhakikisha chupa lote linakaa kwenye mstari, huku akisema kuwa alizingatia zaidi maudhui yatakayotumika kuenda sambamba na ujumbe aliouimba.