Thursday , 2nd Mar , 2017

Msanii Marianne Mdee maarufu kama  'Mimi Mars' ambaye ni mdogo wa msanii Vanessa Mdee amefunguka na kutaja sifa za mwanaume ambaye anahitaji kuwa naye kwenye mahusiano au kuwa mume wake kabisa

Mimi Mars

Mimi Mars akiwa kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio amesema yeye hapendi kuwa kwenye mahusiano na mtu maarufu kama ilivyokwa dada yake na kudai yeye anahitaji mwanaume mpole, ambaye hatakuwa kwenye muziki au sekta yoyote ambayo itamfanya kuwa maarufu.

"Mimi siwezi kutoka na mtu maarufu na namuomba Mungu hilo jambo apishie mbali kabisa, kwani mimi napenda nikiwa na mwanaume au mume nikirudi nyumbani nimkute, awe mpole mpole ila asiwe kwenye mambo haya ya muziki, awe mfanyakazi tu ambaye labda anatoka nyumbani asubuhi na kurudi nyumbani mapema ila asiwe mtu maarufu". Alisisitiza Mimi Mars 

Mbali na hilo msanii huyo amesema kuwa mwezi wa nne anaweza kuachia wimbo wake mwingine baada ya kupokelewa vyema na ngoma yake ya 'Sugar' kwani anadai mashabiki wamekuwa wamkishauri kuwa asikawie kutoa wimbo mwingine.