
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
Katika uzinduzi huo Mbarawa amezionya kampuni za simu kuacha ujanja ujanja utakaowakwamisha wananchi kutumia huduma hiyo mpya.
Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa, mfumo huo ndiyo njia pekee ambayo wananchi wanaweza kuitumia kupima ubora wa huduma za mawasiliano na hivyo ni wajibu kwa kampuni za simu nchini kuhakikisha zinaboresha huduma zake vinginevyo zitapoteza wateja.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba amesema huduma hiyo itahusisha pia miamala ya kifedha inayopatikana kupitia simu za mkononi na hata ile inayounganishwa baina ya mabenki na kampuni za simu kwamba miamala yote itakuwa salama kupitia mfumo huo mpya.