
Ben Pol
Ben Pol akiwa kwenye Planet Bongo ya EATV amewataja wasanii Ibrah Nation, Foby pamoja na Ivra kuwa ni kati ya wasanii ambao anatamani kuwasaida ili kuwavusha kwenye level za juu zaidi kimafanikio.
“Unajua huwezi kusema wazi kuwa unataka kumsaida mtu fulani maana sio kila mtu anahitaji msaada kama unavyodhani ila mimi nadhani kama ni kuwasaida basi ningewasaini Ibrah Nation, Ivra na jamaa mmoja hivi kaimba nyimbo ya mimi ni staa nadhani anaitwa Foby hivyo nadhani hao ndiyo ninaotamani sana kuwasaidia”. Alisema Benpol
Aidha msanii huyo ameweka wazi kuwa Rappa Hamorappa alimpigia simu wiki mbili zilizopita hivyo kitu chochote kinaweza kutokea kuanzia sasa.