Thursday , 26th Jan , 2017

Msanii wa muziki Injili Tanzania Christina Shusho amefunguka na kusema yeye hawezi kuzungumzia tatizo la njaa Tanzania kwa kuwa hajakutana nalo na yeye anaishi maisha ya kawaida ya kila siku hivyo hawezi kusema kama kuna njaa.

Christina Shusho Kikaangoni

Christina Shusho alisema hayo kupitia kipindi cha Kikaangoni ambacho kinaruka kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni kupitia ukurasa wa facebook wa EATV.

"Sijakutana nalo tatizo la njaa hivyo siwezi kulizungumzia, sijaona njaa kwani mimi naishi maisha niliyozoea kuishi siku zote" alisema Christina Shusho 

Mbali na hilo Christina Shusho  amesema yeye hana mpango wa kuja kuwa mwanasiasa na siku zote yeye huwa wanatoa support kwa kiongozi ambaye yupo madarakani kwa wakati huo kwani anaamini hawezi kuwa na marais wa wili kwa wakati mmoja.