
Hiyo ni kwa mujibu wa utabiri uliotolewa mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana (2016) na mtabiri maarufu na mtaalamu wa masuala ya nyota, anayejulikana kwa jina la Maalim Hassan, alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live, cha EATV.
Maalim alisema mambo hayo yatatokea kwa kuwa mwaka huu umeanza siku ya Jumapili ambayo ni siku ya nyota ya Simba jambo linaloashiria utawala ikimaanisha watawala wengi watakuwa na mafanikio makubwa zaidi na pia watu wengi wa nyota ya Simba wanatarajiwa kufanikiwa zaidi katika masuala yao mbalimbali.
Pia katika mwaka huu safari zitakuwa nyingi, fitna pamoja na ongezeko kubwa la wizi, upepo utakuwa mkali sana ingawa mvua itakuwa ni ya kutosha wakati wavuvi wakitabiriwa uhaba mkubwa wa samaki.
Pia Maalim ametoa utabiri kwa upande wa mtu mmoja mmoja