Waziri mkuu wa Tanzania, Mizengo Kayanza Peter Pinda akiwa bungeni mjini Dodoma leo.
Akijibu maswali ya papo kwa hapo leo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda amesema serikali inachukua hatua za dharura kuhakikisha dawa zinazoingizwa nchini zinafaa kwa matumizi ya binadamu ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya usimamizi na ukaguzi katika maduka ya dawa.
Aidha, Mhe. Pinda amezitaka Mamlaka ya Chakula, dawa na vipodozi TFDA pamoja na Shirika la viwango nchini kuongeza kasi ya usimamizi katika kukabaliliana na uingizwaji wa dawa hizo nchini licha ya hatua mbalimbali ambazo mamlaka hizo imekuwa ikichukua.