Alikiba akiwa na tuzo zake alizojizolea leo
Akiongea wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Alikiba alisema yeye ni kama amewashikia tu mashabiki zake kwani tuzo hizo ni zao wao, hivyo aliwashukuru mashabiki kwa kumlinda na mambo mengi ikiwa pamoja na kumuwezesha kuibuka kinara katika tuzo hizo tatu.
"Napenda kuwashukuru sana waandaaji wa tuzo hizi East Africa Televison, napenda kuwashukuru mashabiki zangu maana ninyi mmekuwa mkinilinda kwa mengi, tuzo hizi naweza kusema ni zenu nyinyi na mimi ni kama nimewashikia tu, nashukuru kwa kuniwezesha kushinda tuzo hizi maana bila nyinyi mimi si kitu". Alisema Alikiba.
Alikiba amekuwa msanii wa kwanza katika tuzo za EATV AWARDS kuibuka na tuzo nyingi zaidi kwa upande wa wasanii wa muziki, ikumbukwe pia mwaka jana katika tuzo za Kilimanjaro Music Awards Alikiba alikuwa kinara kwa kujizolea tuzo tano.