Monday , 28th Nov , 2016

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anakabiliwa na uwezekano wa kuadhibiwa tena na Chama cha Soka Uingereza (FA) baada ya kufukuzwa uwanjani na mwamuzi siku ya jana Jumapili, kwenye mechi iliyomalizika sare 1-1 dhidi ya Westham.

Mourinho akiamriwa na mwamuzi kutoka uwanjani katika mchezo wa jana

 

Mreno huyo alifukuzwa na mwamuzi Jon Moss baada ya kuonekana kukerwa na uamuzi wa mwamuzi huyo wa kumuonesha Paul Pogba kadi ya manjano kwa kujiangusha uwanjani ya dhidi ya West Ham, na akapiga chupa teke kwa hasira, wakati Video zimeonesha mchezaji wa West Ham Mark Noble hakumgusa Pogba hata kidogo.

Chama cha soka nchini Uingereza, FA kinasubiri ripoti ya mwamuzi, kabla ya kuamua hatua ya kuchukua dhidi ya Mourinho.

Mourinho, pia alifukuzwa uwanjani mwezi uliopita na mwamuzi Mark Clattenburg wakati wa mechi iliyomalizika sare 0-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Burnley.