Monday , 28th Nov , 2016

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu amesema yuko kwenye mazungumzo na wawakilishi wa klabu moja ya ligi kuu barani Ulaya na mambo yatakapokamilika ataweka hadharani.

Thomas Ulimwengu

 

Ulimwengu amesema mapema sana kuzungumza chochote, kwa sababu bado hajaafikiana na timu anayofanya nayo mazungumzo.

Ulimwengu yupo nchini tangu mapema mwezi huu baada ya kuhitimisha miaka yake mitano ya kuitumikia klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na sasa anashughulikia mipango ya kuhamia Ulaya