Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika viwanja vya Mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika chuoni Bingo kibaha Mkoani Pwani, katikati ni Mkuu wa chuo hicho Mizengo Peter Pinda na kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi ,Tekinolojia na mafunzo ya ufundi Prof. Joyce Lazaro Ndalichako
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Novemba, 2016 katika sherehe za mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania zilizofanyika Bungo, Kibaha Mkoani Pwani.
Kabla ya Rais Magufuli kutoa kauli hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Prof. Elifas Tozo Bisanda alieleza kuwa chuo hicho kimeshindwa kudahili idadi kubwa ya wanafunzi baada ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kuzuia udahili wa wanafunzi wanaotaka kujiunga na masomo ya elimu ya juu kwa kutumia sifa ya kupatiwa kozi ya awali (Foundation Course) ambayo imekuwa ikitumiwa na wanafunzi wasio na sifa za kujiunga vyuo vikuu kwa vigezo vya TCU.
"Kwa vile mnachukuliwa sawa na vyuo vingine ni lazima mzingatie vigezo vya mtu kuitwa mhitimu wa Chuo Kikuu, kwa hiyo nasema kwa dhati nakubaliana sana tena kwa asilimia 100 na yale yaliyozungumzwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia na baadhi ya wahadhiri wa chuo hicho katika Mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika chuoni Bingo kibaha Mkoani Pwani
"Kwa hiyo ni lazima hili suala la kuweka viwango vya ubora wa elimu yetu tulizingatie, ni mara kumi tuwe na wanafunzi hata 10 wanaohitimu elimu ya juu kuliko kuwa na wanafunzi 20,000 wakati hawana sifa, kwa sababu tutakapokwenda kwenye ajira hatutauliza kama huyu ametoka Chuo Kikuu Huria, huyu ametoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ama huyu ametoka Chuo Kikuu cha Dodoma, wote tutawaangalia kwa usawa.
"Tusitafute njia ya mkato, njia ya mkato ni mbaya, kwa hiyo kwa hili kwa kweli Mhe. Prof. Ndalichako nakubaliana na wewe, nafikiri ndio maana umekuwa Waziri wa Elimu, tunataka kulinda hadhi ya elimu yetu" amesema Dkt. Magufuli.
Hata hivyo, Rais Magufuli amekipongeza Chuo Kikuu Huria kwa kazi nzuri ya kutoa elimu ya juu kwa Watanzania wengi na kuanzisha matawi katika nchi mbalimbali za Afrika na ameahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuunga mkono juhudi hizo ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto za miundombinu na mahitaji mengine.
Mkuu wa Chuo hicho Mizengo Peter Pinda akitunuku Shahada, Stashahada na Vyeti mbalimbali vya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika Mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu hicho yaliyofanyika chuoni Bingo kibaha Mkoani Pwani Novemba 24,2016
Katika Mahafali hayo, Mkuu wa Chuo Kikuu Huria na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amewatunuku shahada na vyeti jumla ya wahitimu 4038, wakiwemo wahitimu 8 wa shahada ya Uzamivu, 217 wa shahada ya Uzamili, 111 wa Stashahada ya Uzamili, 1,186 wa Shahada ya Kwanza, 484 wa Stashahada na 1,421 wa vyeti mbalimbali.