
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema, ligi hiyo itachezwa mpaka mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu ambapo itaenda kwa mapumziko kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili.
Lucas amesema, ligi hiyo itamaliza mzunguko wa kwanza mwishoni mwa Desemba kutokana na kupelekwa mbele kwa ratiba mara baada ya timu ya taifa kuwa katika maandalizi ya mechi dhidi ya Cameroon.
Amesema, ligi hiyo bado inahitaji sapoti ya wadau mbalimbali wa soka hapa nchini ili kuweza kufikia katika malengo ikiwa ni pamoja na kuweza kupata zawadi kwa bingwa wa michuano hiyo pamoja na kupata vipaji bora zaidi ambavyo vitaisaidia pia timu ya taifa.