Baadhi ya wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba
UCHAGUZI mkuu wa Simba SC sasa umepangwa kufanyika Juni 29 mwaka huu baada ya tarehe iliyokuwa imepangwa awali Mei 3 mwaka huu kupanguliwa.
Tarehe hiyo ilibadilishwa baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Michezo na Klabu kukataa kuipitisha Katiba ya klabu hiyo iliyofanyiwa marekebisho hivi karibuni.
Kuchelewa kwa uchaguzi huo kunaufanya uongozi wa sasa chini ya Rais Ismail Aden Rage kuzidisha muda wake wa miaka minne tangu Mei 10, 2010 unaomalizika Mei 10 mwaka huu, (Jumamosi ijayo).
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za makao makuu ya Simba SC zilizopo mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam leo (May 7, 2014), Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Damas Ndumbaro amesema kamati yake iliyokutana jijini Dar es Salaam jana, imeamua uchaguzi huo ufanyike Juni 29 kupata Rais, Makamu wa Rais na wajumbe wa kamati mpya ya utendaji ya Simba.
Ratiba ya Mchakato kamili wa uchaguzi huo ni kama ifuatavyo...
Mei 9, 2014: Kwanzaa kutoa fomu
Mei 14, 2014: Kurudisha fomu
Mei 17, 2014: Uhakiki wa fomu za wagombea
Mei 19, 2014: Kutangaza majina ya wagombea
Mei 20, 2014: Kupokea pingamizi dhidi ya wagombea
Mei 25, 2014: Kusikiliza pingamizi
Mei 27, 2014: Usaili wa wagombea
Mei 29, 2014: Kutangaza matokeo ya usaili
Mei 30, 2014: Masula ya kimaadili
Juni 2-9, 2014: Kukata rufaa kamati ya rufaa
Juni 2-7, 2014: Maamuzi ya kamati ya maadili
Juni 10-12, 2014: Kusikiliza rufaa Juni 8-12
Juni 16, 2014: Kukata rufaa kamati ya rufaa ya maadili
Juni 16-20, 2014: Maamuzi ya mwisho ya kamati ya rufaa na kamati ya rufaa ya maadili
Juni 21-23, 2014: Kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea
Juni 24-28, 2014: Kampeni
Juni 29, 2014: Uchaguzi mkuu