
Nape Nnauye
Waziri Nape amesema, mfumo huo utakuwa na changamoto katika hatua hizi za awali lakini anaamini utamsaidia kila shabiki wa soka nchini.
Pia amesema atahakikisha anawashughulikia wale wote wenye nia mbaya na mfumo huu ili kuhakikisha wale wote wanaotakiwa kupata mgao wa fedha katika mchezo husika wanafanikiwa kama ilivyopangwa.
Nape amesema, ameagiza wasimamizi wa huduma za utoaji kadi kuhakikisha hapo kesho wanakuwa wa kutosha katika maeneo husika ili kuhakikisha kila mshabiki mwenye nia ya kuingia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuangalia mechi anafanikiwa bila ya tatizo lolote.