
Vijana wakiendelea na kazi ya kilimo shambani.
Ripoti ya shirika hilo imesema fursa ni lazima zitoe muongozo utakaozingatia mahitaji ya wakulima wadogo na zisizohitaji mtazamo wa mapinduzi ya kijani yanayoambatana na matumizi makubwa ya dawa za kilimo na pembejeo zitakazoharibu rutuba ya mashamba.
Ripoti hiyo iitwayo "Zana za kilimo ni ufunguo kwa wakulima wadogo Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara" inaeleza kwamba zana za kilimo au mashine katika karne hii ya 21 ni lazima ziende sanjari na uhifadhi wa mazingira, ziwe na faida kiuchumi, za gharama nafuu, zinazoweza kutumika popote.
Mkurugenzi msaidizi wa FAO Ren wang anasema bila shaka utumiaji wa mashine au zana muafaka ni muhimu katika uzalishaji wa kilimo Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, na kutaweza kubadili maisha ya mamilioni ya watu na uchumi vijijini.
Hivi sasa theluthi mbili ya zana za uzalishaji wa kilimo zinazotumika katika eneo hilo la Afrika ni msuli wa binadamu.