Wednesday , 21st Sep , 2016

Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam inatarajiwa kukusanya shilingi bilioni 60 kwa mwaka badala ya shilingi bilioni sita za sasa ikiwa ni ongezeko la mara kumi ya makusanyo ya sasa.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Jiji, Siporah Liana wakati wa kongamano la kujadili matumzi ya mfumo wa habari za kijiografia (GIS), ili kuboresha miundombinu ya kusanyaji mapato katika halmashauri ya jiji.

Bi. Liana amesema mfumo wa GIS ni mfumo wa habari unatoumika ulimwenguni kote katika kusaidia ukuaji endelevu wa miji na shughuli zake zote.

Ameongeza kuwa kuboreshwa na kuanza kutumika kwa mfumo huo ipasavyo kutaongeza mapato na kupunguza uchakachuaji wa mapato halisi yanayotakiwa kukusanywa.

Kwa upande wake mtaalam wa mfumo huo Bi. Grace Kyaruzi amesema serikali imeona umuhimu wa teknolojia na kusisitiza kutumika katika sekta mbalimbali za kimaendeleo kama mapato, Ujenzi, Elimu, Afya, Mazingira, matumizi bora ya ardhi na upangaji miji.