
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Cosmas Mwaisobwa
Akizungumza Jijini Dar es salaam katika KIKAANGONI ya EATV, Mwaisobwa amesema kwamba Bodi ya Mikopo inachokifanya kwa walipaji ni kutoza tozo ya kulinda thamani ya mkopo ambao mnufaika alichukua.
'Tunatoza kiwango cha asilimia 6 ya tozo ya kulinda thamani ya mkopo kiwango ambacho ni tofauti kabisa na riba, ukiangalia benki kwa sasa hivi kuna ambazo zinatoza zinatoza zaidi ya asilimia 20 hivyo sisi kazi yetu tunasaidia kutoa elimu na siyo kunufaika zaidi” Amesema Mwaisobwa.
Aidha Mwaisobwa amesisitiza kwamba kwa wote ambao walichukua mikopo na wanajificha kukwepa kulipa, ni lazima watalipa kwa kuwa uhakiki kwa sasa hivi unafanyika katika maeneo mbalimbali na wakibainika penati ya asilimia 10 itawahusu wote wanaokwepa na kuongeza kwamba wanaojitokeza kulipa kwa hiari watatozwa asilimia 8% ya pato lao kwa mwezi.
Pamoja na hayo bodi hiyo imewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutambua kwamba fedha zinazotakiwa kulipwa ni zote kuanzia za chakula, ada pamoja na fedha za mafunzo kwa vitendo.