
Nembo la CHADEMA
Akitoa salamu za pole kupitia taarifa hii Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA bwana Tumaini Makene amesema chama kinatoa wito kwa watanzania wote katika maeneo yaliyopatwa na tetemeko hilo na wengine kutoka nje ya sehemu hizo, kuguswa na tukio hilo na kuwiwa kuwasaidia waathirika wa tukio hilo katika wakati huu mgumu wa kukabiliana na athari zilizotokana na janga hilo.
Viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali, wabunge, madiwani na wanachama wote wa CHADEMA wataungana na kusaidiana kwa kila hali na wote walioguswa na tukio hilo katika wakati huu mgumu wa kupoteza ndugu, jamaa, marafiki, kusitiri miili ya marehemu, kuuguza majeruhi na kupata hifadhi mbalimbali kwa waliopoteza mali na makazi.