
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema kuwa Rais Magufuli ameahirisha ziara hiyo ili aweze kushughulikia tatizo la tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16, mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa kubomolewa mkoani Kagera.
Kufuatia kuahirisha ziara hiyo Mhe. Rais Dkt. Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kumuwakilisha katika sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia, Edgar Chagwa Lungu
Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa kufanyika kesho tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.