
Majimaji FC
Meneja wa timu ya Majimaji FC Godfrey Mvula amesema wamejipanga kwa ajili ya ushindi na kwa upande wao Yanga wanaiangalia kama timu ya kawaida hivyo kazi waliyoifanya ni kurekebisha makosa yaliyokuwa yakijitokeza katika mechi zilizopita ili kuhakikisha lengo lao linatimia.
Wakati Majimaji ikipambana na Yanga katika Uwanja wa Uhuru, Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani itapigwa 'dabi' ya maafande wa JKT Ruvu dhidi ya Ruvu Shooting ambapo Afisa Habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema, wamejipanga kwa ajili ya kupambana na kupata pointi tatu japo wanaamini mchezo huo utakuwa ni mgumu kutokana na kila timu kujiandaa kwa ajili ya kushinda.
Michezo mingine itakayopigwa hapo kesho ni Azam FC watakuwa ugenini dhidi ya Mbeya City mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku Ndanda FC ikiwakaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Nangwanda sijaona Mjini Mtwara.