Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA),Ephraim Mgawe,
Mgawe alibainisha hao jana Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu Cyprian Mkeha, wakati akitoa utetezi wa madai ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa zabuni kwa kampuni ya China Communication Construction Company Ltd(CCCCL).
Magawe amesema kuwa alisaini makubaliano ya kibishara na kampuni hiyo na siyo mktaba wa ujenzi wa gati namba 13 na 14 katika bandari ya Dar es Salaam kama inavyodaiwa.
Akiongozwa na Wakili wake Frank Mwalongo, Mkurugenzi huyo wa Zamani amesema kuwa TPA ilitangaza zabuni ya kupata upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa gati hizo ambapo ilipatikana kampuni ya CPCS ya nchini Canada.
Amesema kuwa baada ya kufanya upembuzi yakinifu ilibainika kuwa ujenzi huo utagharimu Dola za Marekani milioni 321 na kupendekeza kwamba ujenzi huo uwe wa ubia ndipo walipoingia mkataba na CCCCL ambayo iliahidi kufanikisha upatikanaji wa mkopo.