Thursday , 23rd Jun , 2016

Kuelekea katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe, Meneja wa timu ya Yanga Hafeedh Salehe amesema,wachezaji watatu wapo katika mazoezi mepesi kutokana na kutokuwa vizuri kiafya.

Nahodha wa Yanga, nadir Haroub Cannavaro

Hafeedh amesema, Nahodha Nadir Haroub Canavaro na kiungo mshambuliaji Said Makapu hali zao hazikuwa nzuri sana kutokana na kuugua malaria pamoja na beki Oscar Joshua ambaye aliyumia katika mchezo wa awali dhidi ya Mo Bejaia na leo wanaendelea na mazoezi mepesai kwa ajili ya kuwaangalia hali zao.

Hafeedh amesema, hali ya wachezaji hao sio mbaya kiasi cha kushindwa kuwa na kikosi pamoja na wanaamini siku zinavyozidi kwenda ndivyo hali zao zitaendelea kuimarika na kuweza kupambana na TP Mazembe.

Hafeedh amesema, kwa ujumla kambi inaendelea vizuri na kila mchezaji yupo katika hari ya mchezo kwa ajili ya kuikabili TP Mazembe Juni 28 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.