Tuesday , 21st Jun , 2016

Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini SSRA, imeamua kupanua wigo wa huduma za hifadhi ya jamii kwa kuanzisha huduma za hifadhi ya jamii kwa makundi ya afya kwa watu ambao hawapo kwenye sekta rasmi.

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa SSRA, Bw. Honorius Nkole amesema, kwa kuanzia watafungua mfuko maalum kwa ajili ya madereva wa daladala na bodaboda kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na huduma za mifuko ya jamii.

Aidha makundi mengine yatakayonufaika na mfuko huo ni pamoja na mama lishe na madereva daladala ambapo wataweza kunufaika na mafao ya uzeeni, matibabu pamoja na mikopo itajkayowawezesha kukuza mitaji yao.