Wednesday , 15th Jun , 2016

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamadi amesema yeye hana uwezo wa kumrudisha Prof. Ibrahimu Lipumba katika wadhifa wake wa uenyekiti.

Maalim Seif ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalumu na Kituo cha habari cha Sauti ya Amerika.

‘’Yeye alijiuzulu mwenyewe miezi 8 iliyopita hakulazimishwa na alipotaka kujiuzulu watu wengi wakiwamo viongozi wa dini na wazee walimwomba asijiuzulu lakini kaendelea na msimamo wake barua yake niliipokea nikaipeleka katika baraza kuu la viongozi CUF''- Amesema Maalim Seif

Maalim ameongeza kuwa Kufuatia barua hiyo ya kujiuzulu kwa Prof Lipumba baraza kuu la uongozi liliunda kamati ya uongozi kusaidia kuongoza chama hadi hapo atakapochanguliwa mwenyekiti mwingine mpya.