
Naibu Waziri Kamwele ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Mjini Abood Abdul-Aziz aliyetaka kujua mkakati wa serikali wa kuwawezesha wananchi wa Morogoro kuondokana na kero ya maji.
''Serikali imetenga zaidi ya bilioni 4 kwa ajili ya kusambaza maji katika manispaa ya Morogoro na shughuli hiyo itaanza baada ya taratibu za kisheria za kutangaza tenda kukamilika na kupata mkandarasi wa kutandaza mabomba ya maji'' Amesema Kamwele.
Aidha Naibu Waziri amewatoa wasiwasi wakazi wa Morogoro Mjini kwamba baada ya mchakato huo kukamilika kazi hiyo itaanza mara moja ili kuwawezesha kupata maji.