Wednesday , 25th May , 2016

Asilimia 50 ya wakazi wa mji wa Mikindani katika Manispaa ya Mtwara hawana vyoo katika Kaya zao hali ambayo inawafanya kuwa hatarini kupatwa na magonjwa ya milipuko ikiwamo kipindupindu.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akiongea na wananchi

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya mpango wa halmashauri wa kujiandaa na kukabiliana na maafa, iliyowahusisha wakuu wa idara za halmashauri za wilaya ya Mtwara na manispaa, mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, amesema wananchi wanatakiwa kubadilika na kuondokana na changamoto hiyo kwa sababu manispaa inakuwa na kuelekea kuwa jiji.

Aidha, amesema mji wa Mtwara na baadhi ya maeneo mengine katika halmashauri itaendelea kukumbwa na janga la mafuriko kila mwaka iwapo hakutakuwa na mikakati kabambe ya kuboresha miundombinu ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa janga hilo.

Amezitaka halmashauri na wadau wake wa maendeleo kushirikiana pamoja katika kutatua changamoto hizo ili zisiweze kujitokeza tena katika kipindi kijacho cha masika.

sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, akiongea kuhusu vyoo