Mashabiki wa timu za Simba na Yanga wakitazama moja ya mechi iliyozikutanisha timu hizo jijini9 Dar es salaam
Ikiwa ni siku Tatu tangu kuhitimishwa kwa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara,baadhi ya mashabiki wa soka nchini wameipongeza klabu ya soka ya Azam kwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo na kuzitaka klabu kongwe za Dar es salaam Young Africans maarufu Yanga na Simba kujifunza kuhimili ushindani kwa maendeleo ya soka nchini.
Akiongea jijini Dar es salaam, mmoja wa mashabiki wakongwa wa klabu ya Yanga, Said Motisha amesema kufanya vizuri kwa timu za Mbeya City pamoja na Azam katika msimu huu kunaamsha ari na morali kwa timu nyingine.
Katika hatua nyingine,kuelekea uchaguzi wa klabu ya Yanga Motisha amewataka wanachama wa klabu hiyo kuchagua viongozi watendaji watakaoongeza ufanisi wa klabu hiyo na kuifanya kuimarika kiushindani katika ligi kuu ya Tanzania Bara pamoja na michezo ya kimataifa.