Wednesday , 4th May , 2016

Serikali mkoani Mara imetangaza mkakati maalum wa kukabiliana na tatizo kubwa la upungufu mkubwa wa chakula mkoani humo huku kila Kaya ikiagizwa kulima ekari mbili za zao la muhogo ikiwa ni njia mojowapo ya kukabiliana na tatizo njaa.

Mkuu wa mkoa wa Mara Bw. Magesa Mulongo

Mkuu wa mkoa wa Mara Bw. Magesa Mulongo, ametangaza mkakati huo wakati akizindua rasmi mpango huo unajulikana kama niache nijilishe mwenyewe huku akiagiza pia Mabaraza ya Madiwani katika Halmashauri za mkoa huo kupokea mpango huo kwa kuhusisha kila kiongozi katika eneo lake kwa ajili ya kuhamasisha utekelezaji wa agizo hilo.

Amesema kama mkuu wa mkoa hayuko tayari tena kuomba msaada wa chakula cha njaa serikalini na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa Kaya ambayo itashindwa kutekeleza agizo hilo.

Kufuatia agizo hilo la mkuu huo wa mkoa wa Mara, Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara limeunga mkono agizo hilo na kutaka viongozi wa vijiji washirikishwe kikamilifu hatua ambayo wamesema itasadia kupambana na atizo la njaa katika maeneo yote ya mkoa wa Mara.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mara bw Magesa Mulongo,akizungumzia ulimaji wa Mihogo