Naibu wa Fedha na Mipango Mhe. Ashantu Kijaji
Akizungumza Bungeni Mjini Dodoma, Naibu wa Fedha na Mipango Mhe. Ashantu Kijaji, amesema hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuongeza mapato ya ndani ya serikali ili kuongeza pato la serikali kwa ujumla.
Mhe. Kijaji alizitaja hatua hizo ni pamoja kubana na kuziba mianya ya ukwepaji kodi ili kuhakikisha kuwa kila anaestahili kulipa kodi analipa kodi stahiki na kupanua wigo wa kodi kwa kutafuta vyanzo vipya.
Aidha Naibu Waziei huyo alitaja hatua nyingine ni kuweka mazingira wezeshi kwa mlipa kodi ili aweze kulipa kodi bila kubughudhiwa na hatimae kuongeza pato la taifa na kuepuka kuendesha miradi kwa fedha za wahisani ambazo zinakua na masharti magumu.
Bi. Ashantu ameongeza kuwa wabunge watambue kuwa hatua hizo zinazochukulwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli na muhimu hivyo kuwaomba wabunge hao wamuunge Mkono.