Tuesday , 3rd May , 2016

Serikali imekiri kuwa wanawake wengi wa vijijini wanakumbana na changamoto ya kupata msaada wa sheria na kusema Wizara ya Katiba na Sheria imeshapeleka mapendekezo ya kutunga sheria ya msaada wa kisheria utakaofanya wanawake wote kupata msaada huo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu

Akiongea Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema katika kipindi kifupi kijacho serikali itakua imeshatunga sheria hiyo ambayo itakua mkombozi wa wanawake wote.

Hata hivyo Mhe. Ummy amesema kuwa licha ya suala hilo kufanyiwa kazi lakini hadi sasa serikali inashirikiana na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali ambayo yanatoa misaada mbalimbali ya kisheria kwa wanawake.

Waziri Ummy alitoa kauli hiyo ya serikali mara baada ya Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Ritha Kabati kutaka kujua ni lini serikali itahakikisha wanawake wanapata msaada wa kisheria hasa waliopo vijijini.

Sauti ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumzia Changamoto za msaada wa kisheria