Friday , 18th Apr , 2014

Waendesha baiskel 6o kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanziba kuchuana hapo kesho katika mbio za kilomita kumi katika mashindano ya wazi Muungano, mashindano yakayoanzia Mwenge kuelekea Chanika na kumalizia fukwe za Coco jijini D'salaam

Moja ya mashindano ya Baiskeli nchini Tanzania

Waendesha baiskel 6o kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanziba kuchuana hapo kesho katika mbio za kilomita kumi katika mashindano ya wazi Muungano,mashindano yakayoanzia Mwenge kuelekea Chanika na kumalia katika fukwe za Coco jijini Dar es salaam.

Akiongea hii leo jijini Dar es salaam, Katibu mkuu wa Chama cha Baiskel Tanzania CHABATA John Machemba amesema tayari wakimbiza baiskeli mbalimbali wameshawasili jijini Dar es salaam tayari kwa mashindano hayo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Machemba amesema mashindano hayo yatahusisha wakimbiza baiskeli kutoka ndani na nje ya nchi ambao wamekwisha shiriki katika mashindano mbalimbali.