Wednesday , 16th Apr , 2014

Mabondia Thomas Mashali na Kalama Nyilawila watapanda ulingoni Mei Mosi mwaka huu kuwania ubingwa wa kimataifa wa UBO katika pambano litakalofanyika kwenye ukumbi wa Karume ndani ya viwanja vya maonesho ya biashara vya mwalimu Julius K Nyerere.

Mashali baada ya kukabidhiwa mkanda katika moja ya mapambano aliyoshinda.

Mabondia Thomas Mashali na Kalama Nyilawila watapanda ulingoni Mei Mosi mwaka huu kuwania ubingwa wa kimataifa wa UBO katika pambano litakalofanyika kwenye ukumbi wa Karume ndani ya viwanja vya maonesho ya biashara vya mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pambano hilo litasimamiwa na Rais wa UBO kwa Afrika, Emmanuel Mlundwa pamoja na TPBO kama wasimamizi wa ndani ambapo Rais wa TPBO Yassin Abdllah Ustaadh maarufu kama Rais bila majeshi amesema kila kitu kitakwenda sawia.

Wakati huo huo, pambano kati ya Francis Miyeyusho na Mohamed Matumla ambalo lilikuwa lifanyike tarehe 26 mwezi huu, limesogezwa mbele mpaka tarehe 10 mwezi ujao ili kumpa nafasi Bondia Francis Miyeyusho muda wa kupumzika baada ya kuwa amepigana na bondia kutoka nchini Thailand tarehe 19 mwezi huu.

Mratibu wa pambano hilo, Ally Mwanzowa amesema amekubali kulisogeza mbele pambano hilo kwa sababu za kimichezo licha ya kwamba Francis Miyeyusho alishasaini kupigana tarehe 26 mwezi huu huku akisema lengo la kuingia katika kusimamia mabondia ni kuinua mchezo huo.