Tuesday , 22nd Mar , 2016

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar e Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi Simon Siro amewataka wakazi wa Dar es salaam kutii agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es laam Paul Makonda la kuhakiki silaha.

Kamanda Sirro ameyasema hayo baada ya kuzihakiki silaha za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye aliwasilisha silaha zake mbili aina ya 'shortgan' na 'pistol'.

Rais Magufuli ameonyesha njia kwa kuwa mtu wa kwanza kutii agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliyetoa siku 90 wananchi kuwasilisha silaha zao kwa jeshi la polisi kwa ajili ya kuzihakiki.

''Agizo hili ni zoezi zuri ambalo litasaidia kuona ni jinsi gani silaha uliyomilikishwa unavyoitumia na elimu pia tutatoa kwa wanaomiliki silaha hizo juu ya matumizi mazuri ya silaha''-Kamanda Siro

Aidha Kamanda Sirro amesema kuwa kwa watu ambao hawatatii agizo hilo ndani ya muda uliopangwa jeshi la polisi lina Inteligensia ya kutosha na silaha kama SMG ,AK 47 haziuzwi popote hivyo kwa watakaokamatwa na silaha ambao hawatazihakiki sheria itachukua mkondo wake.