Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu amesema hayo jana katika viwanja wa mnada wa Ng'ombe vilivyopo mji Mdogo wa Katoro, Mkoani Geita alipokuwa anahitimisha ziara yake mkoani humo na kuwaomba wananchi kuwafichua wahamiaji haramu ambao wanaishi na kununua ardhi kinyume cha utaratibu wa nchi.
Waziri Mkuu majaliwa amewataka watanzania kutambua kuwa nchi ina rasimali nyingi za kutosha hivyo hakuna haja ya kuanza kugombana wenyewe kwa wenyewe hadi wakati mwingine kufikia hauta ya kufanya mauaji kisa kugombani rasimali ambayo kila mtanzania ana haki nayo.
Aidha katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka watumishi wa serikali kufanya kazi zao kwa weledi na kwa manufaa ya wananchi na kamwe hawatamvumilia mtumishi mzembe atakae tumia wadhifa wake kuwanyanyasa wananchi.
Pia Waziri Majaliwa amaewataka wananchi na watumishi wa serikali kwa ujumla kila mmoja kujikita katika shghuli yake kikamilifu kwa lengo la kujileta maendeleo na ndio lengo la kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya Hapa kazi tu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amameliza ziara yake ya kikazi Mkoani Geita na kurejea jijini Dar es Salaam