Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt, Harrison Mwakyembe
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema wamepiga hatua kubwa katika ukamilishaji wa mahakama hiyo na kuwataka Wanainch wasubiri taarifa rasmi ya Serikali ya kuanza kazi kwa Mahakama hiyo.
Dkt. Mwakyembe amesema kuwa kazi ya msingi ya kukamilisha uanzishwaji wa mahakama hiyo imeshakamilika kilichobaki ni kuepeleka vyombo vya juu zaiidi ili iweze kupata baraka huku akibainisha kuwa katika kufanikisha hilo wamemshirikisha Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba.
Akizungumza juu ya uboreshaji wa Mahakama hiyo Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba ambae aliwahi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria miaka ya Nyuma amesema kuwa uanzishwaji wa Mahakama hiyo haitoshi bila kuboresha vyombo vinavyoshirikiana katika uendeshaji wa Kesi.
Jaji Wairoba amesema kuwa suala la uanzishwaji wa Mahakama hiyo ni jambo zuri lakini chombo kimoja hakiwezi kushughulika tatizo hilo pekee yake bila ya kuwepo ushiriki mzuri wa Jeshi la Polisi naTakukuru ambao wanahusika moja kwa moja.