Thursday , 10th Mar , 2016

Mamlaka ya mapato nchini Tanzania TRA imesema itaendelea kusimamia mapato ipasavyo ili kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano katika kuongeza mapato yatakayoiwezesha nchi kujitegemea na kuhakikisha serikali inaweza kuwahudumia wananchi wake.

Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata

Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa ukusanyaji wa mapato, matumizi ya mashine za EFD'S, kusitishwa kwa bei elekezi na usajili wa vyombo vya moto.

Kidata amesema Kwa kipindi cha mwezi Januari 2016 Mamlaka ilikusanya kiasi cha shilingi Trillion 1,079,993.20 kwa Tanzania bara na Zanzibar ambayo ni sawa na asilimia 102 ya lengo la shilingi Trillion 1,059,na Makusanyo haya yametokana na ari na uthubutu ambao TRA imejiwekea katika kusimamia na kuhakikisha inaendelea kuziba mianya ya ukwepaji kodi na kuweka mazingira rafiki kwa mlipakodi.

Aidha Kamishna huyo ameongeza kuwa kwa upande wa usajili wa magari nchini TRA imefanya ukaguzi hivi karibuni, na kubaini kuwepo kwa magari ambayo yaliingizwa nchini na kusajiliwa bila kufuata taratibu za forodha hivyo kuyafanya yamilikiwe bila kulipiwa kodi stahiki.

Amesema tayari mamlaka hiyo imeshwataarifu Wamiliki wa magari hayo tayari wameshataarifiwa kufika TRA kufanyiwa uhakiki ili kuyalipia kodi stahiki.

Kidata ameongeza kuwa hali hiyo inatokana na Utaratibu wa misamaha uliowekwa hapo awali kwa ajili ya kuwapa nafuu wawekezaji ila wahusika amekuwa wakiitumika vibaya kwani magari yameingizwa mengi kuliko mahitaji na kupelekea serikali kukosa mapato.