Waziri wa Ardhi ,nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
Hayo yameelezwa na Waziri huyo katika ziara yake kwenye kijiji cha Loksale wilayani humo ambapo ametangaza kufuta hati za mashamba ya Meru interprises ekari 12000,Alfan Masoud ekari 2276,joel kivuyo ekari 18810.
Lukuvi amesitiza kuwa wawekezaji wasioendeleza ardhi watanyang`anywa na kurudishiwa wananchi ili kutimiza azma ya serikali kuwamilikisha ardhi wananchi.
Afisa Mtendaji wa kata ya Loksale, Abeli Omosi Akisoma Risala kwa niaba ya wananchi amesema kuwa kumekua na uhaba wa malisho kutokana na ardhi kubwa inayomilikiwa na wawekezaji ambayo haiendelezwi,huku Isack Joseph mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli akilalamikia utendaji wa serikali ya mkoa
Wilaya ya Monduli imetakiwa kufanya tathmini ya maeneo ya wawekezaji iwapo yanatumika kulingana na mkataba ,pamoja na kuingizia mapato serikali ili kuhakikisha mpango wa matumizi bora ya Ardhi.