
Moja ya bunduki aina ya SMG iliyokamatwa kutoka katika matukio ya kihalifu
Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi Yussuf Ilembo amesema mbali na kuzikamata silaha hizo, pia polisi imewakamata majambazi watatu ambao wako mikononi mwa polisi na baada ya kupekuliwa wamekutwa na risasi 40 zikiwemo 31 za SMG na silaha nyingine iliyokamatwa ni bastola ikiwa na risasi tisa.
Aidha, amesema pamoja na jitihada zinazochukuliwa na jeshi hilo la polisi Zanzibar, za kukabiliana na matukio ya ujambazi ,bado wananchi wengi hawajapata mwamko wa kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.