Wednesday , 9th Apr , 2014

Mabondia Thomas Mashali na Kalama Nyilawila, wamesaini mkataba wa kupanda ulingoni kuwania ubingwa wa UBO-Continental, katika pambano la raundi 10 litakalofanyika Mei 1,2014, katika ukumbi wa Karume ndani ya viwanja vya maonesho ya Mwalimu Nyerere.

Katika picha hii ya maktaba, bondia Thomas Mashali(kulia) anaonekana akiwa na Yassin Abdallah Ustaadh katika ofisi za TPBO Ltd. Bondia huyo amesaini kupigana na Kalama Nyilawila, Mei Mosi mwaka huu.

Mratibu wa pambano hilo, bwana Yassin Abdallah Ustaadh ambaye ni Rais wa TPBO, amesema mabondia hao wamekuwa wakilitaka pambano hilo kwa muda mrefu kwa hiyo ujio wake ni majibu ya nani mkali baina yao. Mwaka mmoja uliopita, katika ukumbi huo huo na tarehe hiyo hiyo, Tho,as Mashali alipigwa kwa KO na Francis Miyeyusho.

Wakati huo huo, mabondia wengine Mohamed Matumla na Francis Miyeyusho ambao watapanda ulingoni siku April 26 mwezi huu, wanaendelea vizuri na maandalizi yao. Mabondia hao wataoneshana ubabe katika kunogesha sikukuu ya miaka 50 muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mratibu wa pambano hilo, bwana Yasin Abdallah Mwaipaya Ustaadh maarufu kama Rais bila Majeshi amesema hata kwa upande wa waandaaji, kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa.

Pambano linaonekana kuvuka mipaka ya kuwa pambano la kawaida na kuwa vita kati ya Kinondoni anakotoka Francis Miyeyusho aka Chichi Mawe na Temeke anakotoka Mohamed Matumla aka Snake Boy Junior kama anavyoelezea mmoja wa wakaazi wa Kinondoni.